Kiungo wa Chelsea Michael Essien atarejea uwanjani katikati ya mwezi wa Januari baada ya kupona maumivu ya goti yaliyokuwa yakimsumbua kwa muda mrefu.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ghana hajacheza kandanda msimu huu wote baada ya kuumia kabla ya mechi ya kwanza ya kufungua msimu.
Kocha wa Chelsea Andre Villas-Boas amesema Essien anakaribia kupona kabisa ili aweze kucheza mechi akianza katika kikosi cha kwanza.
"Atarejea katika kikosi katikati ya mwezi wa Januari na atakuwa tayari kwa mechi," alisema Villas-Boas.
"Natumai ni wiki tatu tu zimesalia, atakuwa katika nafasi ya kucheza mechi ngumu na akianza katika kikosi."
Essien aliumia goti wakati wa mazoezi ya kujiandaa kwa msimu, ikiwa ni maumivu mapya aliyoyapata muda mfupi tu tangu apone goti ambapo nusura angetundika viatu kabisa na kuacha kandanda.
Amekumbwa na kuumia goti vibaya mara tatu katika kipindi chake cha kuichezea Chelsea.
No comments:
Post a Comment