Tangaza Biashara yako hapa

Sunday, January 1, 2012

Ahadi ya O'Neil kwa Ulimwengu wa Soka

Martin O'Neil na Peter Musembi

Meneja mpya wa Sunderland Martin O’neill anasema mchuano kati yao na Manchester City tarehe mosi Januari utakuwa mtanange wa hakika, na hiyo ni ahadi yake kwa wasikilizaji wa matangazo ya Ulimwengu wa Soka kupitia Idhaa ya Kiswahili ya BBC London. 

Idhaa ya Kiswahili ya BBC itakuwa inatangaza mechi hiyo moja kwa moja kutoka uwanja wa Stadium of Light, mjini Sunderland.

Martin O’neill anafahamu jinsi ligi ya primia ya Uingereza inavyofuatwa sana na mashabiki wengi Afrika mashariki na kati, na pia anafahamu siku hiyo watangazi wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC watakuwa uwanjani kutangaza mchuano wao dhidi ya Man City.

“Naona fahari sana kwamba tunafuatiliwa kutoka maeneo mengi, barani Asia hadi Afrika mashariki. Hili linanipa furaha kubwa, kwa sababu najua Sunderland ni klabu kubwa tangu zamani, ni vile tu vilabu vingine ambavyo vina fedha nyingi vimeipiku,” O’neill aliambia BBC Ulimwengu wa Soka.

‘’Lengo letu ni kuirejesha hadhi ya zamani ya Sunderland, na hiyo inawezekana.” Aliongeza.
Mechi hiyo inatarajiwa kuwa ngumu huku Man City wakipania kukaa kileleni kwenye msimamo wa Ligi, nao Sunderland wakidhamiria kupata matokeo mazuri ili kuimarisha nafasi yao.

Bwana O’neill amewaahidi mashabiki Afrika mashariki kutazamia mchuano mkali.
“Nina hakika kutakuwa na fataki,” alisema.
Kuhusu mshambuliaji wa Ghana Asamoah Gyan ambaye aliondoka klabu hiyo kwenda kucheza Uarabuni kwa mkopo, Bwana Oneil aliiambia BBC angetaka kumrudisha mchezaji huyo katika klabu baada ya kipindi cha mkopo, lakini akasema hatua kama hiyo itategemea Gyan mwenyewe, klabu anayoichezea na pia bodi inayosimamia Sunderland.

Wachezaji kutoka Afrika waliosalia katika Sunderland ni Stephane Sessognon kutoka Benin, na Ahmed Almohamady kutoka Misri.

Benin na Misri hazikufuzu kushiriki fainali za kombe la mataifa ya Afrika, na hii inampa furaha Martin Oneill kwamba wachezaji wake hawataondoka mwezi Januari kwenda kuwakilisha mataifa yao katika fainali hizo zinazoandaliwa kwa pamoja na Gabon na Equatorial Guinea.

“Ni furaha kwa sababu sitahitaji kupoteza wachezaji hawa muhimu kwa kipindi cha mwezi mmoja, na tutakapokuwa na mechi ngumu hiyo haitakuwa sababu yoyoye ya kuwa na wasi wasi.”

Michael Essien kurejea uwanjani Januari

Kiungo wa Chelsea Michael Essien atarejea uwanjani katikati ya mwezi wa Januari baada ya kupona maumivu ya goti yaliyokuwa yakimsumbua kwa muda mrefu.
Michael Essien kurejea uwanjani mwezi wa Januari
Michael Essien akiongea na vyombo vya habari
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ghana hajacheza kandanda msimu huu wote baada ya kuumia kabla ya mechi ya kwanza ya kufungua msimu.

Kocha wa Chelsea Andre Villas-Boas amesema Essien anakaribia kupona kabisa ili aweze kucheza mechi akianza katika kikosi cha kwanza.

"Atarejea katika kikosi katikati ya mwezi wa Januari na atakuwa tayari kwa mechi," alisema Villas-Boas.
"Natumai ni wiki tatu tu zimesalia, atakuwa katika nafasi ya kucheza mechi ngumu na akianza katika kikosi."
Essien aliumia goti wakati wa mazoezi ya kujiandaa kwa msimu, ikiwa ni maumivu mapya aliyoyapata muda mfupi tu tangu apone goti ambapo nusura angetundika viatu kabisa na kuacha kandanda.
Amekumbwa na kuumia goti vibaya mara tatu katika kipindi chake cha kuichezea Chelsea.

Twaweza: Long walk to ending gender violence

 The 16-day global activism against gender based violence ended recently with the marking of the International Human Rights Day. This year’s theme was “For everyone, for every day in every way, let’s stop any kind of violence against women.”

The aim was also to highlight the key roles that women play in the family and the society in general. In Tanzania, support for women’s issues is one of the priorities of government as well as non-governmental agencies.
The campaign drew the attention of policy makers, governments and civil society, to advocate for the elimination of all forms of violence against women and foster community rights development organizations.
HakiMadini under the ‘We Can’ campaign “Twaweza” has been organising various activities in Arusha as part of the 16-day activism in collaboration with district alliances, organisations, change makers and institutions since last year. This year, the event was marked on November 30 at the Blue Fame Triple A .
Activists focused attention on the issue that violence against women is one of the most widespread of human rights abuses. It includes physical, sexual, psychological and economic abuse, cutting across boundaries of age, race, culture, wealth and geography.
It takes place at home, on the streets, in schools, the workplace, in farm fields, refugee camps, and especially during conflicts and crises. Its manifestations range from the most universally prevalent forms of domestic and sexual violence to harmful practices, abuse during pregnancy and other types of femicide.
Globally, six out of every ten women experience physical and/or sexual violence at one time or another. A World Health Organization study of 24,000 women in 10 countries found that the prevalence of physical and/or sexual violence by a partner varied from 15 percent in urban Japan to 71 percent in rural Ethiopia, with most areas being in the 30-60 percent range.
When people think of spousal abuse, the danger lies in criminalising all men and hating them for their violent nature, yet surely not all men are violent.
The Tanzanian population is estimated to be 44.7 million as for July 2011. Almost half of the population is under 15 years which makes it about 21 million people.
Roughly in every three people only one is a man. That gives the ratio of two to one. Simply, this means that we are talking about seven million men - potentially violent, which can be translated into a lot of cases of physical domestic abuse.
There are many reasons one can give for violent actions by men, though they can never be justified. But the bottom line should be that at any cost should be change our ways and mainly culture by challenging and changing social attitudes, behaviour and practices that engender violence against women.
“In association with the Twaweza national alliance’s mandate to facilitate and create networks for action, our programme will be organised in partnership with various institutions. Working in partnership ensures that domestic violence remains everyone’s responsibility,” said David Mtiruka, acting director of Haki Madini.
Two years of the “Twaweza” camping in Arusha Region focused on awareness and creating change makers, at the same time clarifying obligations of the state to prevent, eradicate and punish violence against women. However, the continued prevalence of violence against women demonstrates that this global pandemic of alarming proportions must continue to be attacked with creative new strategies.
“Violence against women and girls has far-reaching consequences, harming families and communities. For women and girls aged between 16 - 44 years, violence is a major cause of death and disability. In 1994, a World Bank study on ten selected risk factors facing women in this age group found rape and domestic violence more dangerous than cancer, motor vehicle accidents, war and malaria.
Studies also reveal increasing links between violence against women and HIV and Aids. A survey among 1,366 African women who live in Africa including Tanzania showed that women who were beaten by their partners were 48 percent more likely to be infected with HIV than those who were not,” said the northern zone project manager of the “Twaweza,” campaign, Eliamani Rassia.
The Twaweza campaign has made some progress in addressing violence against women in Arusha, Manyara and Kilimanjaro and it has contributed to instituted national plans of action.
However, gaps still remain as there are no specific legal provisions against domestic violence, while marital rape is not a prosecutable offence in Tanzania, he pointed out.
“Observations relevant to research, policy and service provision enabled us to have a general picture of the nature of the problem behind violence against women in the zone. Some of the problems identified are structural, cultural and others social, all posing challenges to the media and others in addressing the matter.
A solution to conflict, as proposed by one of interviewed activists, is to discuss all differences before they blow out of proportion.
“When things get too hot and complicated, I prefer to walk away from the situation and come back to it after they have calmed down,” he added.

Saturday, December 24, 2011

Tshisekedi ajiapisha nyumbani kwake DRC

Kiongozi wa upinzani Etienne Tshisekedi amejiapisha mwenyewe nyumbani kwake baada ya kuzuiliwa kutoka nyumbani.
Majeshi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yameziba njia ya kwenda kwenye uwanja wa michezo ambapo kiongozi mkuu wa upinzani alipanga kujiapisha.
Etienne Tshisekedi amekataa kukubaliana na ushindi rasmi wa Rais Joseph Kabila katika uchaguzi uliofanyika Novemba.
Mwandishi wa BBC Thomas Hubert kwenye mji mkuu, Kinshasa alisema kuna ulinizi wa hali ya juu katika uwanja huo.
Lakini msemaji wa Bw Tshisekedi aliiambia BBC kiongozi huyo wa UDPS bado alikuwa na nia ya kujiapisha.
Rais Kabila aliapishwa kwa muhula wa pili siku ya Jumanne kufuatia kutangazwa kuwa mshindi rasmi baada ya kupata asilimia 49 ya kura zote, ukilinganisha na asilimia 32 za Bw Thisekedi.
Waangalizi kutoka nchi za kimagharibi walitoa shutuma kwamba matokeo hayo ya urais yana mapungufu makubwa, lakini tume ya uchaguzi- inayoungwa mkono na umoja wa Afrika- ulisifia uchaguzi huo kuwa na mafanikio.
Shirika la kutetea haki za binadamu lenye makao yake makuu Marekani Human Rights Watch (HRW) limesema polisi wameua takriban watu 24 tangu uchaguzi huo wenye utata kufanyika.


Etienne Tshisekedi

Siku ya Alhamisi, chama cha Union for Democracy and Social Progress cha Bw Tshisekedi kilituma kwa kile kinachoonekana mialiko rasmi kwenye karatasi zenye anuani rasmi, ikitaka waandishi wa habari na wanadiplomasia kuhudhuria sehrehe za kuapishwa kwake siku ya Ijumaa asubuhi.
Lakini mwandishi wetu alisema alikataliwa kuingia kwenye uwanja huo wa michezo na barabara zote zinazozunguka makazi ya Bw Tshisekedi kwenye mji mkuu zimewekewa vizuizi.
Kulingana na shirika la habari la AFP, polisi wametumia mabomu ya kutoa machozi kusambaza wafuasi wa upinzani waliozunguka nyumba hiyo.
Polisi na jeshi wote wamesambazwa kwenye uwanja wa Martyr mjini Kinshasa, ambapo ni ngome ya upinzani, mwandishi wetu alisema.
Vifaru, mabomba ya maji na askari wenye bunduki na maguruneti nao walionekana.
Mwandishi wetu alisema, polisi wamewakamata watu kadhaa wakati walipojaribu kuingia unwajani humo.
Wanadiplomasia wamekuwa wakisistiza kuwepo na majadiliano juu ya uchaguzi huo, lakini watu kadhaa wamefariki dunia katika ghasia zilizotokea mjini Kinsahsa na maeneo mengine yaliyo ngome za upinzani tangu uchaguzi uanze.
Uchaguzi wa Novemba ulikuwa wa pili DRC tangu vita vya 1998-2003, vilivyosababisha vifo vya watu takriban milioni nne.
Siku ya Alhamis, tume ya uchaguzi ilisimamisha uhesabuji wa kura za wabunge, ikisema inahitaji msaada wa kimataifa kukamilisha hatua hiyo kufuatia madai ya udanganyifu.
Bw Tshisekedi aliongoza kampeni za kuwepo demokrasia chini ya aliyekuwa kiongozi wa nchi hiyo Mobutu Sese Seko lakini huu ni uchaguzi wake wa kwanza kugombea.
Aligomea uchaguzi wa mwanzo wa mwaka 2006, ulioandaliwa chini ya usimamizi wa umoja wa mataifa, baada ya kudai uchaguzi ulifanyiwa hila.
Uchaguzi huo uligubikwa na wiki kadhaa za mapigano mitaani na wafuasi wa mgombea aliyeshindwa, Jean-Pierre Bemba.
Kwa sasa anakabiliwa na kesi katika mahakama ya kimataifa ya ICC kwa madai ya makosa ya uhalifu wa kivita katika nchi jirani ya Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Friday, December 23, 2011

AC Milan na Man City kumjadili Tevez

Makamu Rais wa klabu ya AC Milan Adriano Galliani atafanya mazungumzo na klabu ya Manchester City siku ya Alhamisi juu ya uwezekano wa uhamisho wa Carlos Tevez.
Carlos Tevez akiwa na binti yake Ezeiza nchini Argentina
Carlos Tevez akiwa na binti yake Ezeiza nchini Argentina
Galliani ataelekea Manchester kuzungumzia uhamisho na maafisa wa Manchester City.
Inaaminika Manchester City itamruhusu mshambuliaji huyo kujiunga na Milan kwa mkopo mwezi wa Januari iwapo klabu hiyo ya Italia itatoa uhakikisho wa kumchukua kwa mkataba wa kudumu msimu ujao wa usajili.
Awali Milan ilikuwa tayari kutoa kitita cha euro milioni 23 sawa na paundi milioni 19.3 kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji huyo, lakini vinara hao wa Ligi Kuu ya Kandanda ya England walikataa.
Mabingwa hao wa ligi ya Serie A kwa wiki kadha wamekuwa wakimfuata Tevez, kikwazo kikiwa makubaliano ya uhamisho wake.
Galliani amethibitisha mkutano na Manchester City ulipangwa tangu siku ya Jumatatu.
Amesema: "Siku ya Alhamisi tuna mihadi na Manchester City kuhusiana na suala la Tevez, lakini huenda isiwe kikao kitakachotoa uamuzi wa mwisho wa mazungumzo yetu.
"Hatuendi kumchukua hapo hapo, tutawaeleza tupo tayari kumchukua kwa mkopo na baadae kumnunua mwezi wa Juni.
"Mchezaji mwenyewe anataka kujiunga nasi na si PSG - [Paris St Germain] na tuna matumaini Manchester City wataafiki."
Kwa sasa Tevez yupo kwao Argentina akiwa amekwenda huko bila ya ruhusa ya mwajiri wake tangu mwezi wa Novemba.
Pia amekuwa akihusishwa na klabu ya Paris St Germain, lakini mkurugenzi wa kandanda wa klabu hiyo ya Ufaransa Leonardo amesema hawatapambana na AC Milan iwapo wataweza kukamilisha taratibu za uhamisho wake.
Leonardo, mchezaji na meneja wa zamani wa Milan ameliambia gazeti moja la Ufaransa la La Repubblica: "Sitawaibia Milan Tevez".

Man United yalalamikia mgao wa tikiti

Manchester United imelalamika kwa Chama cha Kandanda cha England -FA- kuhusiana na mgao wao wa tikiti kwa mpambano wa Kombe la FA mzunguko wa tatu mwezi Januari dhidi ya Manchester City.
Uwanja wa Etihad mjini Manchester
Uwanja wa Etihad wa timu ya  Manchester City
Chini ya taratibu za FA, Manchester United wana haki ya kupata mgao wa asilimia 15 ya uwezo wa viti 47,805 katika uwanja wa Etihad, ambao ni sawa na tikiti 7,100.
Hata hivyo, Manchester City imetoa tikiti 5,500, ikiwa ni asilimia 11 tu, hii ni kutokana na sababu za usalama uwanjani.
Manchester United ina mgawanyo maalum kutoka kwa FA, kutokana na uwezo wa uwanja wake wa Old Trafford wenye viti 76,000, kutoa asilimia 11 ya tikiti kwa timu ngeni, sawa na tikiti 8,500.
Mashateni hao Wekundu wanadai wapatiwe mgao wao kamili kwa ajili ya pambano hilo, litakaloanza saa saba mchana siku ya Jumapili tarehe 8 mwezi wa Januari.
Manchester City, ambao kwa sasa wanashikilia usukani wa Ligi Kuu ya England, watawakaribisha mahasimu wao hao wakubwa Manchester United katika mtanange huo wa Kombe la FA kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1955.
Timu hizo zilikutana katika hatua ya nusu fainali mwaka jana kwenye Kombe la FA uwanja wa Wembley, ambapo Manchester City waliibuka washindi kwa bao 1-0 , baadae wakailaza Stoke katika fainali na kufanikiwa kushinda mashindano makubwa kwa mara ya kwanza kwa kipindi cha miaka 35.
Manchester City iliwaadhibu Man United walipokutana mara ya mwisho kwa mabao 6-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England kwenye uwanja wa Old Trafford.

John Terry kufikishwa mahakamani

Nahodha wa Timu ya Taifa ya England John Terry anakabiliwa na mtihani wa kufunguliwa mashtaka ya uhalifu kwa kutumia lugha ya ubaguzi wa rangi dhidi ya mchezaji mwenzake Anton Ferdinand wakati wa mchuano wa Ligi kuu.
Nahodha wa Chelsea
John Terry
Inasemekana kua John Terry alitumia lugha ya ubaguzi wakati wa pambano kati ya klabu ya Chelsea na Queens Park Rangers iliyomalizika kwa ushindiwa QPR mnamo tarehe 23 Oktoba.
Huduma inayohusika na mashtaka(CPS) inasema kua Bw Terry anakabiliwa na mashtaka ya ukiukaji wa sheria ya ubaguzi wa rangi hadharani.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 ameapa kujitahidi kwa ala kulla hali kukabili madai hayo.
Polisi imemhoji mchezaji huyo wa Chelsea kwa tahadhari tangu mwezi Novemba na faili kuhusu suala hilo kutumwa kwenye huduma za mashtaka mwanzoni mwa mwezi huu wa Disemba.
Alison Saunders, Mwanasheria mkuu wa jiji la London, amesema kua ameishauri Polisi ya mji mkuu kumfungulia mashtaka John Terry kwa matamshi yake ya kuchukiza kinyume cha sheria inayohusu ubaguzi wa rangi.
Chama cha mpira, FA kiliahirisha upelelezi wake kikisubiri uwamuzi wa Huduma ya mashtaka ukamilike.
Kutokana na hatua ya hivi sasa Bw.Terry anatarajiwa kufika mbele ya Koti ya Mahakama ya London ya magharibi ifikapo tarehe 1 Febuari.
Akipatikana hatia atatozwa hadi pauni za Uingereza 2,500.
Uwamuzi juu ya kesi ya John Terry unatokea siku moja baada ya mshambuliaji wa klabu ya Liverpool Luis Suarez kuhukumiwa kifungo cha kukosa mechi nane za Ligi kwa kumtukana beki wa klabu ya Manchester United - Patrice Evra.